IFAHAMU VICOBA ONLINE KWA UNDANI
VICOBA (Village Community Bank) ni mfumo wa kuweka na kukopa kwa wanachama waliojiunga kwa pamoja na kuunda kikundi kwa malengo ya kujikwamua kiuchumi. Mfumo huu ulianza Tanzania miaka kumi iliyopita na umeonyesha mafanikio makubwa kwa wanachama wake kuweza kukopeshana, kusaidiana katika matatizo mbalimbali, kuanzisha miradi ya pamoja ya kiuchumi. LENGO/MADHUMUNI YA KUUNDA VICOBA Madhumuni ya kuunda vicoba ni kuunganisha nguvu na rasilimali za wanachama ili kuondoa umaskini na kuleta maendeleo kwa kufanya yafuatayo:- Kuchangia/kununua hisa Kuchangia mfuko wa jamii Kuendesha mfuko wa kuweka na kukopa Kushiriki katika mafunzo ya kuongeza ujuzi wa biashara, uongozi na uanzishaji wa shughuli mbalimbali za pamoja za maendeleo. Kutafuata soko la pamoja na la uhakika kwa bidhaa za wanakikundi Kuna tofauti gani kati ya VICOBA na SACCOS? VICOBA na SACCOS ni vikundi vya kiuchumi vyote vina malengo sawa isipokuwa mfumo wa uendeshaji. 1. Katika VICOBA wanachama uweka